About the Founder of Bwc

Arthur Noeli Mulungu
Mchungaji Arthur Mulungu ni Mtumishi aliyempokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wake Mwaka 1998 katika huduma hii ya TCRC ambapo alianza kuukulia wokovu kwa kuhudhuria mafundisho ya kitume na ibada zenye nguvu za Roho Mtakatifu. Alianza kumjua Mungu hatua kwa hatua na mwaka 2006 Mungu alimjalia kufunga ndoa yake takatifu na Exaveria Mulungu ambao waliendelea kumtumikia Mungu kwa mafanikio makubwa sana ndani na nje ya kanisa wakifanyika baraka sana kwa watu wengi. Mwaka 2008 Mungu alimpaka mafuta rasmi kwa kusimikwa kuwa mmojawapo wa wachungaji waliokuwa wanafanya kazi na Askofu kanisa mama pale Mabibo Dar Es salaam. Hata hivyo baada ya kutumika takribani miaka 10 kama Mchungaji msaidizi Mungu alikuwa anasema nae juu ya kuanzisha huduma ambapo mnamo tarehe 09 December 2018 yeye na mke wake waliweza kufungua tawi la huduma hii likianzia nyumbani kwao Goba Dar Es salaam. Kwa sasa wamefanikiwa kujenga nyumba ya Mungu eneo la Mageti Goba ambapo mpaka sasa wana washirika takribani 100.
Your Sighting for Comming year - 2023
Namna bora ya Kuyaishi Mafanikio na Bwana
Mchungaji Arthur na Exaveria Mulungu wote ni waalimu kwa taaluma kwa hiyo huduma yao imejengwa katika kuamini kufundisha neno la Mungu la kweli na hivyo wanaamini baada ya kumjua Mungu wa kweli ndipo unaweza ukamwabudu ipasavyo. Kauli mbiu ya huduma hii ni BWC (Bethlehem Worship Centre) yaani kituo ama mahali ambapo neno la Mungu la kweli linahubiriwa na mwisho kumwabudu Mungu katika roho na kweli na hivyo waumini kuwa na afya ya kiroho kuelekea mafanikio ya kiroho na kimwili.
Huduma ya BWC hutekeleza maono makubwa ya TCRC ambapo huamini katika kuhubiri neno la Mungu la kweli kutapelekea kuwa na waumini wenye kumjua Mungu kikamilifu na hawa ndio wataweza kumtumikia Mungu katika kicho chake yaani watamwabudu katika roho na kweli, wataishi maisha matakatifu, Watakuwa ni mabalozi wazuri wa kuhubiri Injili ya kweli na mwisho ni kuwa na kanisa lenye Nguvu za Mungu katika kuwabariki waumini wake baraka za mwilini na za rohoni, "Ayubu 22:21 Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia".
Mwito wa Mchungaji kwa kanisa ni; Kukuchunga na kukujenga uwe mkristo Imara mwenye Mahusiano binafsi na Mungu ama kuwa na ukaribu na Mungu ya kwamba Mungu anayemjua Mchungaji wako uweze kumjua ikiwezekana zaidi ya viwango vyake (vyangu) na hivyo ukishamjua Mungu na kuwa na mahusiano ya karibu hakika atakusaidia kibinafsi. Mkristo asiye na mahusiano na Mungu akipata makwazo hawezi mtegemea Mungu na ataanguka; Mchungaji hupenda wakristo wasiweke Tumaini kwake bali waamini katika kumtegemea Mungu na wawe nae kikamilifu nae atajifunua katika maisha yao.
Kuifahamu Huduma hii; Maana Kamili ya BWC [Soma makala hii]
Bethlehem Worship Centre