The founder of the Ministry

Deogratias Rwetaka
Mtu wa Mungu, Mtumimishi Deogratias Rwetaka; Mchungaji na aliyekuwa ni Mwanzilishi na Askofu wa kanisa la Kanisa la Tanzania Christian Revival Centre (TCRC). Mnamo mwaka 1988 akiwa mkoani Iringa akifanya biashara aliamua kumpokea Yesu kuwa bwana mwokozi wake ambapo baadae mwaka huo huo huo aliamua kuhamia Mbeya kufanya kazi za kihandisi kwenye kampuni inayoitwa NOVEC Construction Limited. Baadaye mwaka 1989 alianza kufanya kazi kama Mtumishi wa Mungu na kutambua Mungu amemwita. Mnamo 1990 alianza kufikiria jinsi ya kuanzisha huduma yake ingawa alikuwa anatumika chini ya Huduma iliyo chini ya Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT),Lililokuwa limeanzishwa na kusimamiwa na Askofu Dr. Moses Kulola. Mnamo mwaka 1993 Mungu aliweka mzigo mkubwa sana wa Kufundisha huduma tano akizunguuka nchi za Afrika Mashariki, Amerika na Ulaya. Katika kuendelea kutumikia, Mungu alijifahamu hasa mwaka 1995 kama Mtume na baadae mwaka huo huo alioa mke anayeitwa Lugano Rwetaka ambaye baada ya harusi walihamia Dar es salaam. Mungu amewabariki watoto watatu; Jenipha, Ruth na Erick..
Katika mipango yake ya kuanzisha huduma, mwaka 2015 alianzisha kanisa ama huduma ya Kitume na ya Uamsho iitwayo TCRC na hivyo kutokuwa chini ya mwanvuli tena. Huduma hii inapatikana Mabibo Relini karibu na AMI, Barabara ya Mandela - Dar es salaam. Kanisa tangu kuanzishwa kwake limekuwa kwa kasi afrika ya mashariki na kuwa na matawi zaidi ya kumi (10) katika nchi za Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi.

Askofu Lugano Rwetaka
Katika mipango yake ya kuanzisha huduma, mwaka 2015 alianzisha kanisa ama huduma ya Kitume na ya Uamsho iitwayo TCRC. Huduma hii inapatikana Mabibo Relini karibu na AMI, Barabara ya Mandela - Dar es salaam. Kanisa tangu kuanzishwa kwake limekuwa kwa kasi Afrika ya mashariki na kuwa na zaid ya 10 nchini Tanzania Uganda, Rwanda na Burundi.
Mnamo Tarehe 18 May 2020 Kwa neema ya Bwana Mungu alimtwaa kupitia ajali mbaya ya gari Askofu na mwanzilishi wa huduma hii ambayo baadae bodi ya juu ya kanisa ilikaa na kumpitisha mke wake Lugano Rwetaka kuwa ndiye askofu mkuu. Ayubu 1:21 akasema, Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nili uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile; Bwana alitoa, na Bwana ametwaa; jina la Bwana na libarikiwe.
Mwishoni mwa enzi wa uhai wake, alikuwa akisisitiza sana upendo na mshikamano katika kufanya kazi ya Mungu na zaidi kuwafikia watu wasiokuwa na wokovu waweze kuwa na wokovu. Alikuwa na mzigo wa kulea vipawa vya watu na alipenda kuwapa nafasi watumishi wote katika fursa ya kumtumikia Mungu, Tumuenzi kwa kuyafanya yale aliyoanzisha. Zaburi 133:1-3 Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza, Ndugu wakae pamoja, kwa umoja. Ni kama mafuta mazuri kichwani, Yashukayo ndevuni, ndevu za Haruni, Yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake. Kama umande wa Hermoni ushukao milimani pa Sayuni. Maana ndiko Bwana alikoamuru baraka, Naam, uzima hata milele.
MKwa sasa askofu Lugano Rwetaka ndiye Askofu Mkuu Tanzania na Katibu wake ni Mchungaji John Msigwa anayechunga Tawi la Kanisa hilo lililoko Matosa. Ofisi kuu ya Askofu Lugano ni KANISA la Mahali Pamoja na MABIBO ambapo anatumika na wachungaji wasaidizi wawili kwa majina; Peter Tembo na Ibrahimu Johnathan .
Bethlehem Worship Centre