• Bethlehem Worship Centre Church; Goba Mageti, Dar es salaam

project-slider-image
project-slider-image
project-slider-image
project-slider-image
project-slider-image
project-slider-image
project-slider-image
project-slider-image
project-slider-image

Huduma ya kanisa la BWC ipo kukuunganisha na Mungu

Kanisa hili huamini katika kufundisha kwenye Neno La Mungu La Kweli na Kufanya Ibada Zenye Uwepo Wa Roho Mtakatifu ambazo huleta mguso wenye kuleta majibu katika maisha yao. Tangu huduma hii ianzishwe, Ni miaka minne sasa lakini ukuaji wake ni wa hali ya juu sana kwani mpaka sasa tunamwona Mungu katika ukuaji kiroho, Ustawi wa ujenzi wa Mahali pa kuabudia, watu kupokea baraka za Mungu, wengi kupokea miujiza yao, Kuinuliwa katika Uchumi wa mtu mmoja mmoja na ukuaji wa watumishi kuinuliwa na Bwana katika karama na Vipawa.

Huduma yetu mpaka sasa tumekwisha ifikia jamii yetu na kuishirikisha Upendo wa Mungu,Wapo waliokutana na Mkono wa Bwana kupitia kuitikia wito wa Kuokoka na wamefunguliwa vifungo vyao na kuanza kuuona mkono wa bwana kwa Baraka. Jiunge nasi kumpokea Yesu na kuwa Mwanafamilia ya Ufalme wa Mungu kupitia kanisa la Bwc, Tubarikiwe sote.