• Bethlehem Worship Centre Church; Goba Mageti, Dar es salaam

Huduma za Kiroho

BWC ni kanisa la Kipentekoste linaloendesha huduma za kiroho likijikita kwenye mambo matatu makubwa; Neno la Mungu, Maombi, Sifa na Kumwabudu Mungu kama njia bora ya kumwona Mungu na Kubarikiwa kiroho na Kimwili. Karibu Uabudu nasi na Tubarikiwe Pamoja.

Huduma ya BWC ni wazo la Serikali ya Mbinguni, Lililowekwa kwa Mtumishi wa Mungu ARTHUR NOELI MULUNGU litekelezwe yaani kuanzisha Kituo cha Mungu duniani kwa ajili ya kukutana na watu wote katika nyanja za Kiroho na Kimwili. Mpaka sasa watu wengi wamekutana na Mungu kwa Baraka tele; Uponyaji, Miujiza, Mafanikio, Vipawa na Karama na Matokeo yake chanya ni Ukuaji na ustawi wa Kanisa kwa kasi sana.

project-slider-image
project-slider-image
project-slider-image
project-slider-image

What Makes Us Different?

Jamii ya wakristo wengi wa sasa wameendelea kuishi kwa maisha ya mashaka na kutokufikia lengo lao na la Mungu pia kwamba wafanikiwe. Matokeo wamejikuta wanaangukia kwenye Imani potofu ambazo zimewatesa na kuwaletea majanga na umasikini mkubwa kwa kuwapa vyakula visivyofaa, Bwc imewekeza katika:-

  • Ushirika wa Mtu na Mungu ni wa msingi.
  • Maisha Matakatifu na Kumhofu Mungu.
  • Kuliishi neno la Mungu siku zote.
  • Kuwaandaa watumishi wa leo na kesho.
  • Ndoa ni Taasisi muhimu katika Jamii na Kanisa.

what you should know?

Tunaamini kwa Mungu wa Kweli aliyefunuliwa kupitia neno lake Takatifu.

Anguko la Asili ya Kumwasi Mungu ambapo Mwanadamu alihitaji kuokolewa na Mungu kwa Mpango wa Msalaba.

Maamuzi ya Mwanadamu kumwamini Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wake.

Kufikia malengo ulijiwekea na kupata Kibali kwa Mungu katika kukufanikisha ambapo matokeo yake lazima iwe ni Amani na Furaha.

Umependezwa na Huduma yetu?